Share

AMRI YA MAHAKAMA: WABUNGE WATATU WA CHADEMA WAKAMATWA

Share This:

Wabunge watatu wa CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa amri ya wabunge wa 4 wa chama hicho wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Wabunge waliokamatwa ni wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Osterbay.

Heche na Msingwa wamekamatwa leo mara baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuonana na Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza kesi inayowakabili, Thomas Simba.

Leave a Comment