Share

Anayedaiwa kumzushia Magufuli kwenye Facebook arudi tena mahakamani

Share This:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepiga kalenda kesi ya Mfanyabiashara Henry Munis (30) anayedaiwa kuchapisha taarifa za uongo dhidi ya Rais John Magufuli na kuzisambaza katika Facebook.

Shauri hilo limeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa serikali Saada Mohammed kueleza kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Baada ya kueleza hayo, shauri hilo limeahirishwa hadi March 6, 2019. Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, inadaiwa kuwa Desemba 28,2018 katika maeneo ya Veta jijini Mbeya mshtakiwa Munis alichapisha taarifa katika ukurasa wake wa facebook kuwa ‘Jinsi Magufuli alivyochota Trilion 1.5 za ATCL akitumia ujanja wa kuleta ndege ili atuibie ‘ huku akijua taarifa hizo ni za uongo zenye nia ya kuupotosha umma.

Leave a Comment