Share

Bangi yapatikana na kung’olewa South B

Share This:

http://www.swahilihub.com
MSHUKIWA aliyedaiwa kupanda bangi katika shamba karibu na kampuni ya Express Kenya karibu na mto Ngong, tarafani South B jijini Nairobi alikwepa mtego wa kunaswa na maafisa wa usalama.

Hata hivyo, naibu wa chifu wa Land Mawe, Bw Famau Ali akishirikiana na wazee kutoka mitaa ya Mukuru-Kaiyaba na Mukuru-Commercial walivamia shamba hilo na kungo’a bangi iliyopandwa humo shambani.

Bw Famau alisema aligundua kuna shamba la bangi wakati alikuwa akishika doria mitaani anakofanya kazi.

Aliongeza kwamba mimea hiyo ilikuwa imetafunwa na ng’ombe kwani ilikuwa imechanganyikana na mimea mingine.

Kibarua hicho hakikuwa rahisi na kilichukua zaidi ya saa mbili kufanyika.

Kulikuwa na changamoto kwani mimea ya bangi ilikuwa imepandwa karibu na mto huku ikiwa vigumu kwao kuing’oa wakiongopa kutumbukia mtoni.

Bw Famau aliomba wananchi kushirikiana na utawala pamoja na polisi kutoa habari ndiposa wahalifu wakamatwe.

Licha ya hayo alitoa onyo kwa wazazi amabao watapatikana na hatia ya kutopeleka watoto wao shuleni kwamba watakamatwa.

Kuhusu mshukiwa aliyetoroka, alionya kwamba chuma chao kiko motoni na siku zake arobanne ziko karibu kufika.

Leave a Comment