Share

BIBI AHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KUMUUA MJUKUU

Share This:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Mfanyabiashara Ester Lymo (47), baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia mjukuu wake Naomi John (7).

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashitaka na utetezi.

Amesema kuwa baada ya kujiridhisha pasina kuacha shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka amemtia hatiani Lyimo kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Naomi John.

“Hukumu ya kosa la mauaji ni moja tu ni kunyongwa hadi kufa,” amesema.

Leave a Comment