Share

BREAKING: Ajali ilivyoua Askari 10 wa JKT, 25 wamejeruhiwa muda huu Mbeya

Share This:

Basi lenye namba za usajili T 755 BAB lililokuwa limebeba Wanafunzi wa JKT waliokuwa wanatoka Tabora kuelekea Mbeya kwa ajili ya mafunzo limepinduka katika eneo la Igodima wilayani Chunya mkoani Mbeya na kusababisha vifo vya watu 10.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Mussa Taibu amethibitisha kutoea wa vifo vya watu 10 nakusema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva pamoja na ubovu wa gari.

Leave a Comment