Share

BREAKING: Jeshi polisi DSM wametoa siku 3 kwa Sheikh Ponda kujisalimisha

Share This:

Jana October 11 2017 katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Issa Ponda alikutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuzungumza kuhusu safari yake ya Nairobi nchini Kenya alikokwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Taarifa zilizoripotiwa jana ni kuwa baada ya mkutano huo na wandishi wa habari polisi walifika eneo kwa ajili ya kumkata Sheikh Issa Ponda lakini hawakufanikiwa.

Sasa leo October 12 2017 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema wametoa siku tatu kwa Sheikh Ponda ili kujisalimisha kituo cha polisi na asipojisalimisha watampata sehemu yoyote.

Leave a Comment