Share

BREAKING: Timotheo Wandiba ahukumiwa Miaka 81 jela

Share This:

Leo March 13, 2018 Stori nayokusogezea ni kutoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imemuhukumu miaka 81 jela mfanyabiashara Timotheo Wandiba baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kujipatia fedha ambazo ni Sh.Bilioni 2.1 kwa njia ya udanganyifu.

Mbali ya Wandiba, pia mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wenzake wawili ambao ni Dickson Okololo na Simon Efrem ambao hawakutiwa hatiani.

Akisoma hukumu hiyo kwa niaba ya Hakimu Joyce Minde, Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri amesema washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa 82, ambapo Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 14.

Leave a Comment