Share

DR.MOLLEL ATINGA MOUNT MERU, ATOA MAAGIZO “INAHITAJI MABADILIKO, SAFU IONDOLEWE”

Share This:

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel ameagiza kuondolewa kwa safi ya uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru inayoongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Shafii Msechu ikiwa ni sehemu ya maboresho katika Sekta ya Afya.

Dkt. Mollel ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara katika Hospitali hiyo na kuzungumza na timu ya uendeshaji wa huduma za Afya ya Mkoa ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Wedson Sichalwe katika ofisi za Mganga Mkuu wa Mkoa huyo Jijini Arusha.

“Tumeona kwamba, Hospitali ya Mount Meru inahitaji mabadiliko makubwa sana yakiuongozi, kwa kushirikiana na mamlaka husika, yafanyike haraka sana, kwasababu kuna mambo ya msingi sana yanayogusa Jamii ambayo yanatakiwa kufanywa kwa ustadi wa hali ya juu” alisema Dkt. Mollel.

Leave a Comment