Share

EXCLUSIVE: MSOMI WA DEGREE ANAYEISHI KWA KUPIGA GITA COCO BEACH,NYIMBO MOJA 3,000

Share This:

Maisha ni safari, Dickson Kambutu ni msomi wa Degree ya Sanaa na Elimu, lakini kwa sasa ni mpiga Gita katika Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam akiwa ni muimbaji wa nyimbo za wasaniiI wengine na za kwake.

Maisha yake kwa sasa yapo katika ufukwe huo ambapo anajiingizia kipato kisichopungua 30,000 kulingana na msimu husika ambapo anawaimbia watu nyimbo za wasanii wengine na za kwake kwa kiasi cha Shilingi Elfu tatu kwa nyimbo moja.

Historia yake imeanzia mkoani Morogoro ambapo ndio amazaliwa huko, miaka kadhaa iliyopita aliachana na ajira ya serikali ya Ualimu kutokana na changamoto alizokutana nazo shuleni na kujikuta anakimbilia Dar es Salaam na kuwa Mmachinga wa kuimba muziki maeneo ya Coco Beach.

Leave a Comment