Share

EXCLUSIVE: Msuva baada ya kufunga hat-trick yake ya kwanza kimaifa

Share This:

Mtanzania Simon Msuva anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadida ya Morocco Jumamosi ya Febeuary 10 2018 ameichezea timu yake ya El Jadida game yake ya kwanza ya club Bingwa Afrika dhidi ya Sport Bissau E Benfica ya Guinea Bissau. Msuva alikuwa sehemu ya kikosi cha Difaa El Jadida kilichocheza dhidi ya Sport Bissau E Benfica na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 10-0, kwa upande wa Msuva amefanikiwa kufunga hat-trick katika game hiyo na kuhusika katika upatikanaji wa magoli matatu mengine akitoa pasi mbili za magoli na akisababisha penati.

Leave a Comment