Share

Geita patachimbika: Professor J, Snura na G Nako watema cheche

Share This:

Ikiwa imebaki siku moja Tamasha la sport Music festival kuwasha moto kanda ya ziwa katika kusheherekea sikukuu ya Iddy wasanii wamezungumzia jinsi burudani hiyo itakavyokuwa.

Tamasha hilo la sport music festival ambalo limetua kanda ya ziwa kuhakikisha wakazi hao wanapata burudani ya aina yake katika maeneo ya Geita,Mwanza na kahama.

Ambapo kutakuwa na michezo ya piki piki pili pamoja na magari huku wakisindikizwa na wasanii mbali mbali wa bongo fleva.

Mbunge wa mikumi profesa jay ambaye pia ni msanii wa kizazi kipya akiwataka mashabiki zake waje kumshuhudia akitoa burudani kwao licha ya kuwa kimwa kwa muda mrefu na majukumu ya wananchi wake.

“Tangu niwe mbunge sijafanya shoo kubwa hii ndo ya kwanza nitafanya maajabu kwenu”amesema prof jay.

Nae mama wa chura snura mushi amesema amejipanga kwa kufanya mazoezi licha ya kukaa mwezi mzima wa mfungo bila kufanya shoo.

“Nimewaandalia vitu vingi na vipya mashabiki zangu,nimejipanga kutengeneza vitu vipya tofauti na mlivyovizoea,ntakchokifanya Geita ni tofuti na nitakachofany Mwanza na Kaham”amesema snura.

Huku msanii wa kutoka weusi G, Nako amerudi tena kutoa shoo ya kibabe hivyo akiwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia shangwe la kutosha kutoka kwake.

Burudani hizo zitakazoanzia Geita sikukuu ya Iddy mosi,Mwanza iddy pili na kumalizikia kahama Iddy tatu.

Leave a Comment