Share

Huyu ni Mtanzania/Muafrika Mashariki wa kwanza kupata shavu la Urais kampuni ya Hollywood

Share This:

Muigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka Tanzania, anayefahamika zaidi kupitia filamu ya Going Bongo, Ernest Napoleon, amechukuliwa kusimamia kampuni ya kimataifa ya utengenezaji na usambazaji filamu, D Street Media Group, kama Rais.

Ikiwa na makao makuu yake jijini New York na ofisi mjini Berlin, Cape Town na Buenos Aires, Napoleon atakuwa na cheo cha pili kwa ukubwa baada ya CEO, Dexter Davis kwenye kampuni hiyo.
Napoleon atasimamia zaidi kazi za kampuni hiyo upande wa Afrika na Mashariki ya Kati, japo hiyo haimaanishi kuwa hatohusika na masuala mengine ya kampuni hiyo duniani kote.

Leave a Comment