Share

“JAMBAZI TUTAENDA NAE KIJAMBANZI, UGOMVI WETU NI KWA WANAOTUFANYIA NDIVYO SIVYO” RC KIGOMA

Share This:

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Gen. Emmanuel Maganga amewaonya wananchi Wilayani Kibondo kuacha kuwaingiza nchi kinyemela vibarua kutoka nchi jirani ya Burundi badala yake wafuate utaratibu wa kuomba vibali maalum kutoka kwa Watendaji wa Vijiji, Kata, na Wakuu wa Wilaya ili vibarua hao wajulikane na kufanya kazi kwa utaratibu na kighalali.

Maganga amesema Serikali Mkoani Kigoma imeshaanza kutengeneza utaratibu wa kutoa vibali maalum kwa Vibarua hao kutoka nchi jirani ya Burundi ili waweze kuingia na kufanya kazi za vibarua katika Vijiji na Wialaya zinazpakana na Burundi.

Akizungumza katika soko la wakulima Kibondo Mjini Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brihgedia Gen. Emmanuel Mganga amesema Serikali imeamua kuanzisha utaratibu huo ili kuondoa wimbi la wahamiaji haramu linalopelekea kuwepo kwa matukio mengi ya kihalifu.

Leave a Comment