Share

”KAMA SIO MTANZANIA USIINGIE HUKU SIO ANGA ZAKO,UKICHAGUA MTU MLENDA ITAKULA KWAKO”RC KIGOMA

Share This:

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Mganga amewataka wananchi wa Kijiji cha Malenga kata ya Rugenge Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma kushiriki vyema uchaguzi wa serikali za mitaa na kufata Sheria za Uchaguzi na kuchagua viongozi Bora watakao leta mendeleo katika maeneo yao na Kuwaonya Wananchi wasio wa Nchi ya Tanzania kuvuruga uchaguzi kwa Kugombea katika Kijiji hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ameyasema hayo alipokua akiongea na Wananchi katika soko la ujirani Mwema liitwalo Lugando Mpakani mwa Burundi na Tanzania ambapo linahusisha Nchi mbili kufanya biashara.

Leave a Comment