Share

KATIBU WA CHAMA CHA MABAHARIA “BILA SIFA HIZI UBAHARIA HAUKUFAI”

Share This:

Neno Baharia limeanza kutumika muda mrefu sana lakini siku za hivi karibuni limeonekana kushika kasi na kutumiwa sana mitaani na mitandaoni huku kila mmoja akilitumia kwa style yake iwe kwenye mazungumzo ya kawaida au ya utani, wengine wameenda mbali zaidi na kuanza kutafsiri maana ya Mtu anayestahili kuitwa Baharia kwa vile ambavyo wanaona inafaa na wapo ambao katika kuitengeneza maana halisi ya Baharia wanatumia hata kauli zinazofikirisha.

Lakini unaweza kujiuliza ni nini hasa maana ya Baharia na zipi sifa za yule anayefaa kuitwa Baharia!?.

Kupitia AyoTv na ‘millardayo.com’ tunae Katibu Mkuu wa Chama cha Mabaharia Tanzania Captain Josiah Mwakibuja ambaye licha ya kuwa Katibu wa Chama yeye pia Mjumbe wa Kamati ya kusaidia Matatizo ya Mabaharia Afrika yenye makao yake makuu London Uingereza na pia ni Katibu wa Bodi ya kutoa misaada kwa Mabaharia kama vile ya kiroho, wakati wa misiba n.k, na amekubali kujibu maswali yote yanayohusu Ubaharia.

Leave a Comment