Share

KESI YA CHADEMA: SABABU YA MBOWE NA WENZAKE KUKUMBUSHIWA MASHITAKA

Share This:

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wamefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza wakitokea uraiani baada ya kusota mahabusu takribani miezi 3.

Mbowe na Matiko sambamba na viongozi wengine 7 wa chama hicho wamefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo kwamba kesi imeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Hata hivyo Hakimu Simba alisema kiutaratibu inapaswa washitakiwa wakumbushwe mashitaka yao kwa sababu kesi hiyo ilikuwa kwa Hakimu mwingine Wilbard Mashauri ambaye ameteuliwa kuwa Jaji.

Leave a Comment