Share

KESI YA KITILYA YAIVA: WAZIRI WA FEDHA,MWANASHERIA MKUU WATAJWA

Share This:

Mashahidi 54 akiwemo aliyekuwa Waziri wa fedha na Uchumi Mustafa Mkuro na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Wa Serikali, Fredrick Werema wanatarajiwa kutoa ushahidi wao katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya na wenzake wanne.

Mbali na mashahidi hao pia vielelezo 218 vinatarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi ‘Mahakama ya Mafisadi’ katika kesi hiyo ya Uhujumu uchumi kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon,
Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda na msaidizi wake Alfred Misana ambapo wote wanakabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Leave a Comment