Share

Kesi ya kupinga sheria ya huduma ya vyombo vya habari Mahakamani EAC

Share This:

Baraza la habari Tanzania (MCT) limewasilisha maombi katika mahakama ya Afrika mashariki ya kupinga vipengele kadhaa vya sheria ya huduma ya habari vinavyokiuka mkataba wa habari wa jumuia ya Afrika mashariki

Kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2017 imefunguliwa na Baraza la Habari Tanzania(MCT) , Kituo cha Msaada wa sheria na haki za binadamu (LHRC) na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) wakilalamikia ukandamizaji wa uhuru wa habari .

Akizungumza nje ya mahakama mapema leo,katibu wa baraza la habari Tanzania,Kajubi Mwakajanga ameipongeza mahakama hiyo kwa hatua ya kupokea na kukubali maombi yao ,tayari kwa kuanza utaratibu wa usikilizwaji wa awali.

Amesema kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa April 13,mwaka huu ambapo waleta maombi watapaswa kuleta viapo na baada ya hapo tarehe 14 Mei wajibu maombi ambao ni upande wa serikali watapaswa kuleta utetezi wao

Mwakajubi na wenzake wanaiomba mahakama hiyo itamke kwamba vipengere hivyo vinakiuka mkataba wa jumuia ya Afrika masharika na kuilazimisha serikali kuvifuta kabisa.

Kesi hiyo inasikiliswa na Jopo la majaji wapatao watatu ambao ni jaji kiongozi wa mahakama ya jumuiya ya afrika Mashariki Monika Mugenyi ,Jaji Fakihi Jundu na Jaji Dkt Fustin Ntezi lyayo

Leave a Comment