Share

KESI YA MPEMBA WA MAGUFULI YAPIGWA KALENDA “MAWAKILI HAWAPO”

Share This:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mfanyabiashara Yusufu Ali maarufu ‘Mpemba wa Magufuli’ na wenzake kwa sababu Mawakili wao hawapo.

Washtakiwa hao ni miongoni mwa washitakiwa waliomuandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuomba kukiri mashitaka yao.

Katika kesi hiyo, mbali ya Mpemba washitakiwa wengine ni Charles Mrutu, Benedict Kungwa, Jumanne Chima, Ahmed Nyagongo na Pius Kulagwa.

Leave a Comment