Share

KESI YA NIDA: VILIO VYATAWALA MAHAKAMANI, NDUGU WALALAMIKA

Share This:

Ndugu,Jamaa na Rafiki wa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa NIDA, Dickson Maimu na wenzake watano wanaokabiliwa na mashtaka 100 ikiwemo utakatishaji fedha wa Sh.Bil 1.17 wameangua vilio katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu kesi hiyo haijasomwa katika mahakama ya wazi (Open Court).

Vilio hivyo vilisikika mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally.

Miongoni mwa watu waliokuwa wakilia na kulalamika alidai kuwa kwanini kesi hiyo imesomwa chamber ‘mahakama ya ndani’ badala ya mahakama ya wazi ‘Open Court’ ili na wao wasikie.

Kutokana na hatua hiyo Askari Polisi waliwataka ndugu, rafiki na jamaa hao watawanyike eneo hilo kwa sababu shughuli za mahakama zinaendelea, ambapo walitii agizo hilo na kuondoka.

Leave a Comment