Share

KINYOZI BUBU NA KIZIWI ANAEMILIKI SALOON KIGOMA, UTASHANGAA ANAVYOWASILIANA NA WATEJA WAKE

Share This:

Imezoeleka kuona baadhi ya watu wenye mahitaji maalumu wakitembea barabarani au katika ofisi mbalimbali wakiomba msaada wa fedha au vitu mbalimbali kwa ajili ya kujikimu kimaisha hii ni kutokana na Maisha duni ambayo wamekuwa wakikabili.
Hii imekuwa ni tofauti kwa Shabani Ramadhani Mkazi wa mtaa wa Vamia kata ya Mwanga kusini Manispaa ya kigoma Ujij Mkoani Kigoma ambaye yeye ana ulemavu wa Kuongea na kusikia yani ni BUBU na pia ni kiziwi ambaye licha ya hali yake hiyo bado amekuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya familia yake kupitia shughuli yake ya Ukinyozi.
Shabani ana mke na mtoto mmoja anafanya shughuli yake ya ukinyozi ambayo mpaka sasa ni takribani miaka saba tangu alipoanza lakini cha kusikitisha ni kuwa hakuzaliwa na kiwa na ulemavu wa kusikia ambao anasema kuwa ulemavu huo uianza taratibu alipokuwa mtoto mdogo.

Leave a Comment