Share

KUMEKUCHA KINONDONI: DC CHONGOLO KUINGIA MTAANI NA TRA KUKAGUA KODI

Share This:

Tunayo stori kutokea kwa Mkuu wa wilaya Kinondoni Daniel Chogolo ambapo amesema wilaya hiyo imetoa nafasi kwa wananchi juu ya ulipaji wa kodi ya majengo na mabango bila faini.

Amesema wameamua kuzindua kampeni ambayo itaanza baada ya wiki mbili ambapo watapita nyumba hadi nyumba kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa ulipaji kodi kwani wakiacha italimbikiza riba kubwa na kuwa mzigo kwa wananchi.

Amesema wanafanya hivyo kutokana na maagizo ya Rais John Magufuli ambapo ametaka Watanzania wapunguziwe kodi ya majengo ambapo kwa mtu mwenye nyumba ya kawaida analipa shilingi 10000, huku mwenye ghorofa analipa shilingi 50,000.

Leave a Comment