Share

Maamuzi ya Mbunge Munde Tambwe baada ya shule kuungua moto

Share This:

Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Tabora Munde Tambwe ametoa msaada wa mifuko 50 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa shule ya Sekondari Kazima ambayo iliungua moto tangu mwezi June mwaka huu.

Sambamba na hilo Munde pia alikabidhi mifuko 100 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa uzio wa Zahanati ya Town Clinic iliyopo mkoani humo pamoja na mifuko 50 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Igalula wilaya ya Uyui.

Leave a Comment