Share

Mabinti watatu wasanii waliofanya wimbo Sema kuwakomboa mtoto wa kike wafunguka

Share This:

Katika maeneo mengi ya Tanzania bado kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambapo wasichana wengi wamekuwa wakiolewa katika umri mdogo, wengine wakibakwa na wengine kupata ujauzito huku wakiwa bado wanafunzi. Hili ni janga kubwa lakini bado wasanii wengi wamekuwa wakilikaushia, ila kwa ujasiri na kuthubutu, mabinti hawa wameamua KUSEMA na kulizungumzia. Wimbo ambao umezalishwa na Tanzania Bora Initiative na Producer Mocco Genius na video kufanywa na Hascana. Tembelea link https://www.youtube.com/watch?v=DIT5PNHrcng kuona video hii. Okoa mtoto wa kike, okoa jamii.

Leave a Comment