Share

Magoli 8 aliyofunga Usengimana anayedaiwa kasajiliwa na Singida kwa zaidi ya Tsh Milioni 200

Share This:

Jina la Danny Usengima kwa soka la Rwanda sio geni lakini kwa Tanzania inawezekana ndio ukawa unalisika kwa sasa baada ya club ya Singida United ya Tanzania kutangaza kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili akitokea club ya Polisi FC inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda. Danny Usingimana ndio mfungaji bora wa Ligi Kuu Rwanda msimu uliyomalizika amefunga jumla ya magoli 19, kuanzia msimu ujao utamuona akicheza Singida United ambao hawajaweka wazi kiasi walichomsajili. Staa huyo anayeitumikia pia timu ya taifa ya Rwanda mitandao rwanda-foot.com wa Rwanda umeripoti kuwa staa huyo wa Rwanda, amesajiliwa kwa dola 100,ooo za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200.

Leave a Comment