Share

MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA NA POLISI DSM

Share This:

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm limesema kuwa limefanikiwa kuwaua majambazi wawili ambao hawajafahamika majina yao na kukamata silaha mbili zikiwa na risasi tano ndani ya magazine walizokuwa wanatumia majambazi hao katika majibizano ya risasi kati yao na askari.
Mnamo tarehe 01/07/2019 majira ya saa nane na nusu mchana huko maeneo ya Kitunda Machimbo kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na majambazi kikiwa maeneo hayo kwa ajili ya kufuatilia majambazi sugu kilikutana uso kwa uso na majambazi wawili ambao walianza kuwarushia risasi baada ya kubaini kuwa wamezingirwa na askari.
Silaha walizokuwa wakitumia majambazi hao ni Bastola mbili aina ya
Browning yenye namba ya usajili A.558816 iliyokuwa na risasi tatu ndani ya magazine na nyingine yenye namba A.963815 TZCAR 101418 ikiwa na risasimbili ndani ya magazine

Leave a Comment