Share

Mauaji Cameroon: Kuwasaka wanajeshi waliomuua mwanamke huyu

Share This:

Mnamo Julai 2018 kanda ya video inayotisha ilisambaa katika mitandao ya kijamii.

Inawaonyesha wanawake wawili na watoto wawili wakielekezwa huku wakiwa wamehsikiwa bunduki na kundi la wanajeshi wa Cameroon.

Wamefungwa macho, wanalazimishwa kukaa chini na wanapigwa risasi mara 22.

Serikali ya Cameroon awali ilipuuzilia mbali video hiyo ikidai ni ‘habari za uongo.’ Lakini BBC Africa Eye, kupitia uchunguzi wa ushahidi wa video hii, inaweza kuthibitisha ni sehemu ipi hasaa mauaji haya yalipotokea, wakati gani, na ni nani anayehusika na mauaji haya.

Uchunguzi wa Aliaume Leroy na Ben Strick

Imesimamiwa na Daniel Adamson na Aliaume Leroy

Msanifu michoro: Tom Flannery

Leave a Comment