Share

Mtandao wa Wanafunzi wachukua hatua nzito baada ya mwenzao kupotea

Share This:

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) umesema mwenyekiti wake Mahmud Abdul Ormari Nondo ahajulikani alipo na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha anapatikana akiwa salama kwa haraka.

Baba mdogo wa kiongozi huyo Mussa Mitumba akiwahutubia wanahabari pia ametoa wito kwa ‘mwanawe’ kurudishwa akiwa hai aendelee na kutafuta kutimiza ndoto zake.

Kiongozi huyo wa wanafunzi alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nvhini humo, Tahliso.

Leave a Comment