Share

Mtanzania anaeshika namba 3 Marekani ktk kampuni za usafirishaji

Share This:

Kutana na Godwin, Kijana Mtanzania ambae amekua akiishi na kufanya kazi Marekani kwa miaka mingi ambapo ameanzisha kampuni ya usafirishaji kwa kutumia teknolojia.

Kampuni yake inaitwa Moovn na kwa Tanzania imeshaanza kufanya kazi na inatumia teknolojia kurahisisha upatikanaji wa usafiri kama Tax, Bodaboda na Bajaji.

Ni kwa kudownload APP yake kwenye simu na inakufanya uepuke kujaza namba za simu za Madereva Tax, pia inakufanya uwe salama zaidi kujua ni Dereva gani anakuendesha, jina lake, picha yake, anapoishi na namba za gari.

Popote pale ulipo Dar es salaam ukihitaji usafiri ukiingia tu kwenye APP utawezeshwa kuona Magari, Bajaji au Bodaboda zilizo karibu na eneo lako.

Leave a Comment