Share

Mufti Zuberi awalipua Diamond na Harmonize kisa muziki wakati wa Iftar

Share This:

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi amewataka waislamu ambao wanawafturisha waislamu wenzao waliofunga kufuata taratibu za dini na kuacha kufanya mambo ambayo yapo kinyume na taratibu. Ameyasema hayo Jumapili hii katika Mashindano ya Kuhifadhi Quran Tukufu yaliyofanyika Diamond Jubilee ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Katika Iftar ya Harmonize iliyofanyika wiki iliyopita, muimbaji huyo alifanya show ya kutambulisha wimbo wake mpya kitu ambacho kimeibua hisia kwa waislamu.

Leave a Comment