Share

“NAMSIMAMISHA KAZI HUYU MHANDISI, HAFAI” -WAZIRI MKUU

Share This:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya ya Morogoro, Brown Undule baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ikiwemo usimamizi mbovu wa ujenzi wa kituo cha afya Mkuyuni.

Amemsinamisha kazi Mhandisi huyo leo Jumatano, Septemba 18, 2019, baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro na kusema hajaridhishwa na aina ya milango iliyotumika.

Waziri Mkuu amesema aina ya milango iliyowekwa katika kituo hicho cha afya haiwezi kutumika hata kwenye nyumba ya mtu binafsi, lakini kutokana na uangalizi mbovu kutoka kwa watendaji walikubali kuweka milango hiyo mibovu.

Amesema Serikali imeamua kujenga vituo vya afya vitano kwenye wilaya hiyo ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi na kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, hivyo watendaji wasimamie ipasavyo miradi hiyo.

Leave a Comment