Share

Ni kweli aliyeifunga Angola alipimwa dawa za kuongeza nguvu

Share This:

Moja kati ya stori ambazo zilichukua headlines jioni ya jana Tanzania ni kuhusiana na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys kudaiwa kuwa alipimwa na viongozi wa CAF kama alitumia dawa za kuongeza nguvu baada ya mchezo dhidi ya Angola. Abdul Hamis Selemani ambaye ndio alikuwa karipotiwa kuwa alikwenda kupimwa kwa kushukiwa kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu kutokana na uwezo wake mkubwa aliounesha katika game dhidi ya Angola licha ya kutoka majeruhi na kuifungia Serengeti Boys goli la ushindi na baadae kuibuka mchezaji bora wa mechi.

Leave a Comment