Share

Nyumba ya Mjane yapingwa mnada bila taarifa, atua kwa RC Makonda

Share This:

Mama mjane ambaye ni mama wa watoto watatu amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuamka asuburi na kukuta nyumba yake iliyopo kwenye plot namba 239 Block B mtaa kwa Kondo, Mbezi, ikipigwa mnada bila kuwa na taarifa yoyote.

Mama huyo ambaye anatambulika wa jina la Benadetha Ruyendela, amedai sehemu hiyo ya kiwanja aliyojenga aliinunua kutoka kwa Bi. Zainabu J Kaswaka na dokomenti zote anazo.

“Kusema kweli sina jinsi kama mnavyoniona mimi ni mjane, hii nyumba ambayo imepigwa mnada kimagumashi ni yangu. Mwaka 2014 nilitafuta kiwanja na baadaye nikakutana na huyo Zainabu, akaniambia mimi nakiwanja changu nikuuzie chote nikasema sina pesa, basi ngoja nikukatie sehemu ya hiyo pesa uliyonayo ndio akanikatia hii sehemu iliyoijenga na ikaweka ukuta kama fensi kabisa. Sasa juzi nimeshangaa wamekuja watu wakapiga mnada nyumba yangu wakati mimi sijui chochote ila yule mama aliyeniuzia ndio anajua kumbe kuna mkopo anadaiwa sijui benki,”

Leave a Comment