Share

RPC KIGOMA ”TUMEUA MAJAMBAZI SITA WAKUTWA NA PANGA NA BUNDUKI”

Share This:

Jeshi la Polisi Mkoani kigoma limefanikiwa kuwauwa watu sita wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi katika eneo la Kiduduye barabara ya kueleka Kijiji cha Mabamba wilayani Kibondo na kukamata silaha mbalimbali ikiwemo AK 47,Shortgun ,visu , Mapanga pamoja na magazini tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Martin Otieno ameeleza kuwa tukio hilo limetekelezwa usiku wa kuamkia leo wakati askari walipokuwa katika doria za kawadia ambapo maiti zimehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo.

Leave a Comment