Share

SIKU 59 ZA WAMBURA WA TFF GEREZANI, UPELELEZI WA KESI YAKE HAUJAKAMILIKA

Share This:

Ikiwa ni siku ya 59 leo kwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura kusota gerezani bado upelelezi wa kesi yake haujakamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wambura ametimiza siku 59 baada ya kufikishwa mahakamani hapo February 11, 2019 akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kusomewa mashtaka 17 ikiwemo utakatishaji fedha wa Mil.75.

Wakili wa serikali, Batilda Mushi amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa ila upelelezi haujakamilika.

Wakili Batilda amedai kuwa kuna nyaraka zinafanyiwa kazi kabla ya upelelezi kukamilika na hawawezi kuweka wazi ni nyaraka zipi, hivyo anaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliomba mchakato huo ukamilishwe kwa haraka.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 25, 2019.

Leave a Comment