Share

“Sio sisi tuliomkataa tumepokea barua kutoka Yanga”-Rais wa TFF

Share This:

Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia amefunguka na kueleza kuhusiana na maamuzi ya kamati ya utendaji wa TFF kumuondoa Frank Sanga wa Yanga katika nafasi ya uenyekiti wa bodi ya Ligi. Wallace Karia ameeleza kuwa sio wao TFF ndio wameamua kumuondoa katika nafasi hiyo ila kanuni na sheria ndio zinamn’goa Sanga katika nafasi hiyo, kwani wamepokea barua kutoka Yanga ikithibitisha kuwa Yussuf Manji ndio mwenyekiti wa Yanga na Sanga ni makamu mwenyekiti.

Leave a Comment