Share

Soudy Brown apata dhamana, akamatwa tena

Share This:

Mtangazaji wa Clouds, Soudy Kadio ‘Soudy Brown’ ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu, lakini amerudishwa mahabusu ya kituo cha polisi kati baada ya kukamatwa tena.

Soudy amerudishwa mahabusu ili kuunganishwa na Msanii Maua Sama ambapo watafikishwa tena mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili. Inadaiwa kuwa wanaweza kusomewa mashtaka ya kudhaliliisha fedha kwa kuzikanyaga.

Awali Wakili wa serikali Mkuu Faraja Nguka akishirikiana na wakili Estazia Wilson wamemsomea shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile.

Nguka amedai kuwa kati ya June 11 na September, 2018 ndani ya Dar es Salaam kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shilawadu TV  alitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa huyo alikana na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hata hivyo, wakili Peter Kibala anayemtetea mshtakiwa huyo aliomba mteja wake huyo apewe dhamana kwa sababu shtaka linadhaminika.

Hakimu Rwizile akitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo alimtaka awe na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh.Milioni 2, pia mshtakiwa mwenyewe naye asaini bondi ya Sh.Milioni 2. Mshtakiwa huyo alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi October 18, 2018.

Leave a Comment