Share

SUGU “KUONDOKA MADIWANI 11 NA MEYA TUMEIMARIKA, WENGINE TUMEKULA VICHWA”

Share This:

MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuhama kwa madiwani 11 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wa Jiji la Mbeya akiwemo Meya, David Mwashilindi na Naibu Meya, Fanuel Kyanula waliotimkia Chama cha Mapinduzi (CC), hakujakidhoofisha chama hicho bali kumekiimarisha zaidi.

Akizungumza kwenye Mkutano wa viongozi waandamizi wa Chadema Kanda ya Nyasa na wandishi wa Habari, Sugu alisema madiwani wote walioondoka walikuwa wamekata tamaa ya maisha ya siasa.

Amesema awali baada ya kupata taarifa ya madiwani hao kutimka, alipata wasiwasi kwamba chama hicho kitakuwa kimepoteza mwelekeo lakini alipofanya utafiti mdogo kwenye baadhi ya maeneo alibaini kuwa bado chama hicho kinakubalika kwa wananchi.

Sugu alisema hofu yake ilikuwa kwamba huenda madiwani hao walihama pamoja na wanachama lakini utafiti wake ulibaini kuwa waliondoka peke yao na familia zao na sio wanachama ambao ndio wapiga kura.

Amesema Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji Mwashilindi alikuwa hashiriki kwenye shughuli za Chama hicho kwa muda mrefu kwa maelezo kuwa hata Mkutano Mkuu wa Chadema uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana jijini Dar es salaam hakuhudhuria.

Leave a Comment