Share

Trump amtimua Tillerson

Share This:

Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi Waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson kwa kutoa sababu kuwa walitofautiana kuhusu masuala mbali mbali ikiwemo mzozo wa Korea Kaskazini, mpango wa kinyuklia wa Iran na Urusi. Trump amemteua mkurugenzi wa shirika la Ujasusi CIA Mike Pompeo kuwa waziri mpya wa mambo ya nje. Trump ametangaza kumtimua kazini Tillerson kupitia ukurasa wa Twitter.

Leave a Comment