Share

TUNDU LISSU ALIVYOKOMALIWA NA MAWAKILI 15 WA SERIKALI

Share This:

Mawakili wa Serikali 15 wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba wamewasilisha pingamizi katika Mahakama Kuu kupinga maombi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuhusu ubunge wake.

Lissu amefunguka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya hati dharura, kupitia kwa Kaka yake Alute Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge.

Dk. Mashamba amemueleza Jaji Sirilius Matupa kuwa mapingamizi hayo yana masuala manne ya msingi ikiwemo kuona kama mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikilizwa maombi hayo kama yalivyoletwa.

Pia amedai wameangalia kama mleta maombi ambaye ni Allute Mughwai ana uwezo wa kuleta maombi hayo na kama maombi hayo yameletwa kwenye mahakama yenye mamlaka.

Dk.Mashamba amedai wanaangalia kama nafuu zilizoombwa kwenye mahakama hiyo ni sahihi kuletwa mahakamani au la.

Katika pingamizi hizo, hoja ya kwanza iliwasilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abubakari Mrisha amedai yapo mambo sita ya kuzingatia kwa mleta maombi ikiwemo kuhakikisha maombi yanaletwa ndani ya miezi sita baada ya maamuzi, mahakama kuona haja ya kusikiliza maombi hayo na maombi kuletwa kwa nia njema si kwa lengo la kupotosha au kwa manufaa binafsi.

“Kati ya hayo, jambo moja pekee kwamba maombi haya yako ndani ya muda lakini mengine yamekosekana katika maombi haya. Maombi haya hayakidhi kwa sababu hakuna maamuzi yoyote yaliyoambatanishwa katika maombi haya ili iweze kuyapitia kama kuna haja ya kuilazimisha mamlaka iliyotoa maamuzi kuyaondoa,” alidai Mrisha.

Pia amedai kuwa hakuna maamuzi yaliyoambatanishwa ili mahakamani iweze kuyapitia na kutoa uamuzi kama kwenye kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Alidai kwa mujibu wa Kanuni za Bunge zinaelekeza Mbunge ambaye ataathiriwa na maamuzi anatakiwa kuwasilisha mapingamizi kwa Katibu wa Bunge ambaye atayawasilisha mapingamizi hayo kwa spika.

Leave a Comment