Share

UTANI WA WAZIRI JAFO: DC JOKATAE NI MZURI SANA, NILISEMA WAKALETA NONGWA

Share This:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe, Jumamosi hii alitembelea ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ambayo inajengwa na kampeni ya Tokomeza Zero kupitia Harambee ambayo ilifanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Waziri baada ya kuona ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia 70, alimpongeza DC Jokate huku akidai ni mmoja kati ya wakuu wa wilaya ambao wanafanya kazi kubwa nchini Tanzania.

Pia alimtaka Mkurugenzi wa Kisarawe, shule huyo ambayo mpaka sasa ina madarasa nane ya kisasa, maabara moja, bweni moja la wanafunzi 100 pamoja na nyumba moja ya mwalimu kuipa jina la Jokate Girl Secondary kutokana kazi kubwa iliyofanya na mkuu huyo wa wilaya.

Leave a Comment