Share

VIGOGO CHADEMA WAKWAMA KUJITETEA

Share This:

Viongozi 9 wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe wameshindwa kuanza kujitetea katika kesi ya uchochezi inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu mawakili wanaowatetea wanasimamia kesi Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 24 na 27, mwaka huu. Leo viongozi hao 9 walitarajia kuanza kujitetea baada ya Mahakama hiyo kuwakuta na kesi ya kujibu kutokana na ushahidi wa mashahidi 8 uliofungwa na Upande wa Mashitaka.

Katika uamuzi wake kutokana na mvutano juu ya ahirisho la kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema amezingatia hoja za pande zote mbili hususani ya upande wa mashitaka ambao umedai Mawakili wao wana kesi mahakama nyingine, pia baadhi ya washitakiwa wamefiwa.

Hakimu Simba amesema anaamini hati za wito zilizotolewa mahakamani hapo ni sahihi na kwa maelezo ya mshitakiwa Peter Msigwa amefiwa na bibi yake mkoani Iringa na John Heche amefiwa na mtoto wa kaka yake Musoma.

“Kutokana na sababu hizi inanilazimu kuahirisha kesi hii lakini siridhishwi kuahirisha kesi kwa siku 20 kwa sababu wakili hajatuletea udhibitisho kwamba mawakili wa utetezi watakuwa busy mpaka Oktoba 7 na 10, mwaka huu kama walivyoomba tuahirishe lakini pia kuna jopo la mawakili wengi katika kesi hii,” amesema Hakimu Simba.

Amesema shauri limekuwa likiahirisha mara kwa mara na kusababisha mahakama kulalamikiwa kuchelewesha kesi, hivyo ni lazima wahakikishe wanamaliza kesi kwa wakati.

Amesema migogoro inayotokea imesababisha kesi hiyo ichelewe mpaka sasa pamoja na kwamba ilianza kusikilizwa kwa hakimu mwengine

Leave a Comment