Share

WACHINA WALIOMPA RUSHWA BOSS TRA WAHUKUMIWA “MIL.11 ZINATAIFISHWA”

Share This:

Raia wawili wa China, Zheng Rongman(50) na Ou Ya(47), wamehukumiwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulipa faini ya Sh.Mil 1 kwa kila mmoja baada ya kukiri makosa ya kutoa rushwa.

Pia mahakama hiyo imetaifisha fedha kiasi cha Sh.Mil 11.5 walizotaka kutoa kama rushwa kuwa Mali ya Serikali.

Rongman ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan International Industry  and Trade Co. Ltd na Ya, wamehukumiwa kulipa faini na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani, Huruma Shaidi.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Shaidi, alisema washtakiwa wametiwa hatiani kama walivyoshtakiwa.

Mahakama hii inawahuku kila mmoja kulipa faini ya Sh 1milioni na kiasi cha Dola za Kimarekani 5,000 ambacho ni sawa na Sh.Mil 11.5 ambazo zimetaifishwa na kuwa mali ya

Bwana alidai kuwa washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza na kupitia Kampuni yao, wameweza kutoa ajira kwa watanzania 100 na wana familia inayowategemea.

Akisoma maelezo ya washtakiwa, Wakili kutoka Takukuru, Ipyana Mwakatobe alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

Leave a Comment