Share

Wakazi walalamikia uhaba wa maji Mukuru

Share This:

http://www.swahilihub.com
WAKAZI zaidi ya 20,000 katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kaiyaba ulioko katika tarafa ya South B, Kaunti ya Nairobi wamelalamikia uhaba wa maji.

Aidha, hali sio hali kwani vyoo vimefungwa kufuatia kuadimika kwa bidhaa hiyo muhimu huku wengoine wakikosa kuoga miili yao fauka ya jua kuwaka zaidi.

Kando na wakazi wa Kaiyaba, mtaa jirani wa Mukuru-Maasai Village nao hauna maji na inawalazimu kutembea katika mitaa ya Mukuru-Hazina, Mukuru-Sokoni na kutoka South B madukani.

Hii ni kutokana na madai kwamba tingatinga zinazopanua barabara katika mtaa huo zilibomoa mifereji inayosambaza maji mtaani huo.

Waliohojiwa walisema maji yanayopatikana yanatoka katika mfereji mmoja uliopitia chini ya daraja inayounganisha Kaiyaba na Hazina.

Pia ni mazingira yanayohatarisjha afya ya wakazi kwani kuna uchafu na takataka karibu na pale maji yanapochotwa.

Wachuuzi walitumia fursa hiyo kupandisha bei ya maji kutoka Sh3 hadi Sh20 kwa kila mtungi wa lita 20.

Wahudumu wa afya ya jamii wanahofia kutokea kwa mkurupuku wa maradhi yakiwemo Kuhara, Kutapika, Homa ya Matumbo (Typhoid) na Amoeba.

Uchunguzi wetu ulibaini ya kwamba wenyeji wanatumia karatasi za nailoni kama vyoo kisha wanavitupa nyakati za usiku.

Leave a Comment