Share

WALIOINGIA ANGA ZA WAZIRI KIGWANGALLA, WAFIKISHWA KISUTU

Share This:

Watu sita wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwemo Hassan Likwena maarufu kama NYONI wakikabiliwa na mashtaka manne ikiwamo la kukutwa na vipande 413 vya Meno ya Tembo na viwili ya Kiboko vikiwa na thamani ya Sh.Bilioni 4.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamis Kigwangalla kutangaza kukamata vipande 413 vya Meno ya Tembo pamoja na NYONI ambaye alimtaja kama mtu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu na Serikali kutokana na kujihusisha na biashara haramu za nyara za Serikali.

Mbali ya Likwena (39) ambaye ni mkazi wa Kivule, wengine ni Bushiri Likwena mkazi wa kitunda, Oliver Mchuwa (35), Salama Mshamu (21), mkazi wa Chamanzi, Haidary Sharifu (44) pamoja na Joyce Thomas (33).

Leave a Comment