Share

WAMBURA WA TFF ALALAMIKIA UPELELEZI MAHAKAMANI

Share This:

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura ameulalamikia upande wa mashitaka kwa kushindwa kutoa taarifa ya upelelezi umefikia wapi.

Wambura alitoa malalamiko hayo mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Alidai tangu Aprili mwaka huu upande wa mashitaka uliahidi kutoa taarifa ya upelelezi lakini mpaka sasa hakuna majibu yoyote kuhusu hatua zilizofikiwa.

Wakili wa Serikali, Ester Martin alidai hajapewa maelekezo yoyote kutoka kwa waajiri wake kwamba alipaswa kutoa maelezo ya upelelezi umefikia wapi hivyo, atafuatilia kujua upelelezi umefikia wapi ili aweze kutoa taarifa rasmi.

Baada ya kueleza hayo, Wambura alidai kama ripoti ya upelelezi ipo tayari inapaswa kutolewa ili mahakamani iweze kufikia maamuzi.

Hata hivyo, Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 4, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Leave a Comment