Share

Wanafunzi wanufaika na jiko la kupika

Share This:

http://www.swahilihub.com
Ni jiko la kisasa litakalowafaidi wanafunzi zaidi ya 300.
Jiko hilo lilijengwa kutokana na pesa za udhamini wa shirika moja nchini.
Bw Etyang aliongeza kwamba wasichana hao watatu walikuwa wametoka katika eneo la Shompole, Kiserian na Ewaso Kedong na walikuwa wenye umri wa kati ya miaka 12 na15.
Kadhalika, walisomea katika shule tatu za msingi zilizoko kwenye maeneo tofauti katika kaunti hiyo.
Alinena kwamba juhudi za serikali kufanikiwa kuwaokoa watoto hao kutokana na ndoa za mapema kulichangiwa na mpango wa nyumba kumi.
“Sina budi kuwaambia ya kwamba mpango wa nyumba kumi ulioshirikisha wakazi na maafisa wa polisi ndio umetuwezesha kuwaokoa watoto hao ambao wana umri wa kati ya miaka 12 na 15,” Bw Etyang akasema.
Aliwashukuru wananchi kwa kupeana habari kwa polisi jambo lililowaongopesha wavunjaji sheria.
Isitoshe, mbali na kutoa habari kwa walinda usalama, polisi wa kushika doria waliongezwa wakati wa sherehe ndiposa usalama ukadhibitiwa.
Akiongea kwenye hafla hiyo, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bw Dennis Ndolo alisema wanafunzi walikuwa na tatizo la mankuli ya mchana kwani hawakuwa na pahali pazuri pa kupikia chakula.
“Mbali na hayo, chumba cha kupikia kilikuwa kidogo na pia moshi ulikuwa ukitutatiza mno,” mpishi aliyedinda kutajwa jina lake akasema.
Mwisho.

Leave a Comment