Share

“WATOTO WANAFUNDISHWA MAMBO YA KIKUBWA NA KUWAPETIPETI WANAUME”

Share This:

Itakumbukwa Siku chache zilizopita @ayotv_ na millardayo.com tulitoa taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro kuanzisha oparesheni ya kusitisha vitendo vya Wazazi kuwapeleka unyago Watoto wao wa kike wenye miaka 5 hadi 14, huku akidai anasitisha vitendo hivyo kwakuwa Watoto wanafundishwa mambo ya kikubwa na kuwafanya washindwe kumudu vema masomo yao huku wakichochewa kuanza ngono wakiwa wadogo na hata kupelekea kushamiri kwa mimba za utotoni.
_
Sasa Founder wa Taasisi ya kupigania haki za Watoto, Vijana na Wanawake ya Tupaze Sauti Foundation, Agness Kahamba amefunga safari hadi Tunduru kujionea hali halisi ilivyo na kupata nafasi ya kuzungumza na Wazazi, Wanafunzi na jamii nzima kwa ujumla kuhusu Shughuli nzima za unyago na leo amekubali kutusimulia yote aliyokutana nayo uko huku akiomba Wadau na Serikali kwa ujumla kuungana pamoja katika kutafuta namna bora ya kutafuta ufumbuzi wa mila hizo.
_
“Kule Tunduru kuna mila fulani imewekwa, Binti akifikisha miaka 14 anapelekwa unyago na wakiwa uko wanafundishwa vitu vya kikubwa, kwahiyo wakitoka wanawaza nimpate mwanaume mwenye hela nimfanyie vile vitu nilivyofundishwa, kwa mwezi wa nane pekee Wanafunzi 23 wa Form IV wamegundulika kuwa na mimba ”
#Millardayo #TupazeSautiFoundation #AgnessKahamba

Leave a Comment