Share

WATUPWA MWEZI MMOJA KOROKORONI KWA KUZAMIA AFRIKA KUSINI

Share This:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu mwezi mmoja Korokoroni na kulipa faini ya Shilingi Elfu Hamsini raia wa Tanzania 52 waliozamia kwenda nchini Afrika Kusini kinyume na sheria.

Hukumu hiyo, imesomwa na Hakimu Mkazi, Victoria Mwaikambo baada ya washitakiwa hao kusomewa mashitaka yao na Mawakili wa Idara ya Uhamiaji Tanzania, Shija Sitta na Godfrey Ngwijo.

Washitakiwa hao walisomewa maelezo ya makosa yao kisha wakakiri mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mwaikambo.

Leave a Comment