Share

Waziri Nchemba amesema hata ukiandamana nyumbani kwako ni kosa

Share This:

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote wanaopanga mipango ya kuandamana.

Mhe. Nchemba ametoa kauli hiyo leo Machi 11, 2018 wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. John Magufuli Mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo leo  amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika maandamano hayo ni kuchafua taswira ya nchi yetu.

“Nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama ya kuua ni kosa, wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi yetu ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma. Watu wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa,”amesema Mwigulu.

Akitilia mkazo sakata hilo, Waziri Nchemba amegusia sakata la mwanafunzi aliyedhaniwa kutekwa siku chache zilizopita, Abdul Nondo, na kumshangaa “Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa. Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?, watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya nchi yetu”

Leave a Comment